JINSI YA KUOMBA (MAOMBI YA HATARI.
EFESO 6:10
Hatimaye ndugumzidi kuwa
hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 11 Vaeni silaha zoteza Mungu,mpate kuweza kuzipinga hila za shetani
Huwa
Mungu amekupa nafasi ya kutambua
kwamba katika wokovu kunayo mambo mengi huwa shetani anapambana na
watu wa Mungu ndiyo maana ya waefeso na hata ukisoma katika HOSEA Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.Namaarifa waliyoyakosa ni kutokujua vita vya kiroho
walivyo navyo dhidi ya shetani na biblia inasema EFESO 4:27 Wala msimpe ibilisi
nafasi.
Mazingira na jinsi ya
kuomba katika muongozo wa Roho Mtakatifu na vipengele vyakuombea
Jinsi Ya Kuomba Maombi Haya
Si Lazima Upige Magoti Unapoomba Maombi Haya, Waweza Kusimama Na Kujiandaa Kama Askari; Unaweza Kuomba Maombi Haya Muda Wa Mchana Au Usiku. Maombi Haya Yanafanyakazi Wakati Wowote Lakini Ni Vyema Zaidi Yawe Wakati Wa Usiku.
Ukumbuke Ya Kuwa; Uhai Na Mauti Vipo Katika Uwezo Wa Ulimi Wako. Mauti Na Uzima Huwa Katika Ulimi (Mithali 18:21), Neno Liko La Uwaza Li Karibu Nawe Sana. Ulikiri Kwa Kinywa Chako Na Moyo, Upate Kulifanya (Kumbu La Torati 30: 14) Kwa Maana, Uwezo Wa Mungu Uko Katika Ulimi Wako Sasa, Tamka Maneno Nayo Yatafanyika. Omba Maombi Haya Haya Maalumu Na Ya Hatari Sana Kwa Shetani Na Majeshi Yake, Omba Katika Nguvu Na Uweza Wa Roho Mtakatifu; Na Shetani Na Majeshi Ya Mapepo Wabaya Yatainua Mikono Juu Kusalimu Amri Mbele Za Uweza Wa Roho Mtakatifu Na Wa Bwana Yesu Kristo Mwana Wa Mungu Aliye Hai.
Uwapo Katika Mashambulizi Makali Ya Kishetani Au Vipingamizi Vikali, Endelea Kwa maana MUNGU bado yupo nawe. Maombi Haya Kuanzia Saa 6.00 Usiku Wa Manane Hadi Saa 9.00 Alfajiri. Kwa Kufanya Hivi, Utawasumbua Na Kuwazuia Maadui Kufanya Mkutano Dhidi Yako Na Wengine Kwa Ujumla ila sio lazima muda huo . Kwa Ajili Ya Usumbufu Huu Utakao Kuwa Unaendelea Kuufanya, Utasababisha Wao Kuliondoa Jina Lako Katika Orodha Ya Wale Wanaotakiwa Kushambuliwa, Kwa Kuondolewa Jina Lako Katika Orodha Ya Wale Wanao Watarajiwakushambuliwa, Na Moja Kwa Moja Utapata Uhuru Na Ufumbuzi Wa Matatizo Yako.
Maombi Haya Hayatosheshi Kukufanya Uombe Kuanzia Usiku Wa Saa 6.00 Hadi Saa 9 Alfajiri Tu, Bali Inabidi Uongeze Maombi Mengine Juu Ya Hayo. Unaweza Kuomba Mara Mbili Au Zaidi Katika Muda Huo Wa Masaa Matatu Ya Maombi Ya Msisitizo (Hiyo Haimaanishi Kwamba Unarudia, Bali Unazidi Kuchochea Moto Zaidi Mahali Ambapo Tayari Pana Moto Dhidi Ya Shetani) Omba Mara Kwa Mara Ukimaanisha Na Kueleweka Ni Nini Unachokisema, Na Kwamba Kweli Umekusudia Iwe Hivyo Ulivyosema.
Ila Epuka Kupaaza Sana Sauti Yako, Ikiwa Upo Kwenye Nyumba Yenye Watu Wengi. Ili Sauti Yako Isije Ikawasumbua Wengine, Hivyo Omba Kwa Sauti Ya Kwaida Na Ya Utulivu, Na Pia Ili Kutunza Siri Ya Maombi Haya Maalumu Sana Na Ya Kivita Na Ya Hatari Sana Kwa Shetani Na Majeshi Yake; Kwani Mawakala Au Wajumbe Wa Shetani Wanaweza Kuwa Wanasikiliza
Jinsi Ya Kuomba Maombi Haya
Si Lazima Upige Magoti Unapoomba Maombi Haya, Waweza Kusimama Na Kujiandaa Kama Askari; Unaweza Kuomba Maombi Haya Muda Wa Mchana Au Usiku. Maombi Haya Yanafanyakazi Wakati Wowote Lakini Ni Vyema Zaidi Yawe Wakati Wa Usiku.
Ukumbuke Ya Kuwa; Uhai Na Mauti Vipo Katika Uwezo Wa Ulimi Wako. Mauti Na Uzima Huwa Katika Ulimi (Mithali 18:21), Neno Liko La Uwaza Li Karibu Nawe Sana. Ulikiri Kwa Kinywa Chako Na Moyo, Upate Kulifanya (Kumbu La Torati 30: 14) Kwa Maana, Uwezo Wa Mungu Uko Katika Ulimi Wako Sasa, Tamka Maneno Nayo Yatafanyika. Omba Maombi Haya Haya Maalumu Na Ya Hatari Sana Kwa Shetani Na Majeshi Yake, Omba Katika Nguvu Na Uweza Wa Roho Mtakatifu; Na Shetani Na Majeshi Ya Mapepo Wabaya Yatainua Mikono Juu Kusalimu Amri Mbele Za Uweza Wa Roho Mtakatifu Na Wa Bwana Yesu Kristo Mwana Wa Mungu Aliye Hai.
Uwapo Katika Mashambulizi Makali Ya Kishetani Au Vipingamizi Vikali, Endelea Kwa maana MUNGU bado yupo nawe. Maombi Haya Kuanzia Saa 6.00 Usiku Wa Manane Hadi Saa 9.00 Alfajiri. Kwa Kufanya Hivi, Utawasumbua Na Kuwazuia Maadui Kufanya Mkutano Dhidi Yako Na Wengine Kwa Ujumla ila sio lazima muda huo . Kwa Ajili Ya Usumbufu Huu Utakao Kuwa Unaendelea Kuufanya, Utasababisha Wao Kuliondoa Jina Lako Katika Orodha Ya Wale Wanaotakiwa Kushambuliwa, Kwa Kuondolewa Jina Lako Katika Orodha Ya Wale Wanao Watarajiwakushambuliwa, Na Moja Kwa Moja Utapata Uhuru Na Ufumbuzi Wa Matatizo Yako.
Maombi Haya Hayatosheshi Kukufanya Uombe Kuanzia Usiku Wa Saa 6.00 Hadi Saa 9 Alfajiri Tu, Bali Inabidi Uongeze Maombi Mengine Juu Ya Hayo. Unaweza Kuomba Mara Mbili Au Zaidi Katika Muda Huo Wa Masaa Matatu Ya Maombi Ya Msisitizo (Hiyo Haimaanishi Kwamba Unarudia, Bali Unazidi Kuchochea Moto Zaidi Mahali Ambapo Tayari Pana Moto Dhidi Ya Shetani) Omba Mara Kwa Mara Ukimaanisha Na Kueleweka Ni Nini Unachokisema, Na Kwamba Kweli Umekusudia Iwe Hivyo Ulivyosema.
Ila Epuka Kupaaza Sana Sauti Yako, Ikiwa Upo Kwenye Nyumba Yenye Watu Wengi. Ili Sauti Yako Isije Ikawasumbua Wengine, Hivyo Omba Kwa Sauti Ya Kwaida Na Ya Utulivu, Na Pia Ili Kutunza Siri Ya Maombi Haya Maalumu Sana Na Ya Kivita Na Ya Hatari Sana Kwa Shetani Na Majeshi Yake; Kwani Mawakala Au Wajumbe Wa Shetani Wanaweza Kuwa Wanasikiliza
Maombi Yako Unapoomba, Maana Ndiyo Kazi Zao.
HATUA ZA MAOMBI MAALUMU KWA NYAKATI HIZI ZA MWISHO.
1. Maandalizi.
a. Ninaomba Neema Yako Ee, Mungu Uliye Hai, Baba Yetu Wa Mbinguni, Uishiye Milele Na Milele, Na Kwa Kupitia Mamlaka Ya Jina Lako, Ee Yesu Kristo Wa Nazareti, Mwana Wa Mungu Uliye Hai, Ninakuomba Utakaso Mbele Zako Ee Mungu Uliye Hai Milele Na Milele, Na Mbele Zako Ee Bwana Yesu Kristo Mwana Wa Mungu Uliye Hai Milele Na Milele, Na Mbele Zako Ee Roho Mtakatifu, Uliye Hai Milele Na Milele, Nami Ninaupokea Utakaso Huu Sasa, Ulioniandalia Kabla Ya Kuwekwa Misingi Ya Ulimwengu, Na Kwa Kifo Chako Ee Bwana Yesu Pale Msalabani, Ninajitakasa Sasa Na Hata Milele Kwa Utakaso Huu Kwa Damu Ya Yesu Kristo Mwana Wa Mungu, Uliye Hai Milele Na Milele, Na Kwa Utakaso Huu Kwa Neno La Mungu Uliye Hai Milele Na Milele, Na Kwa Utakaso Huu Kwa Upako Wa Roho Mtakatifu Wa Mungu Uliye Hai Milele Na Milele; Na Kwa Utakaso Huu Kwa Jina La Yesu Kristo Wa Nazareti, Mwana Wa Mungu Uliye Hai, Uishiye Milele Na Milele! Na Kwa Utakaso Huu Ninazifisha Nguvu Zote Za Kila Aina Ya Dhambi, Na Kila Aina Ya Uchungu Wa Dhambi, Na Kila Aina Ya Magonjwa, Na Kila Aina Ya Udhaifu, Na Mauti. Na Kwa Utakaso Huu Ninang’oa Kila Aina Ya Pando Lisilopandwa Na Baba, Mungu Uliye Hai, Katika Jina La Yesu Kristo Mwana Wa Mungu Uliye Hai Milele Na Milele, Amina!
HATUA ZA MAOMBI MAALUMU KWA NYAKATI HIZI ZA MWISHO.
1. Maandalizi.
a. Ninaomba Neema Yako Ee, Mungu Uliye Hai, Baba Yetu Wa Mbinguni, Uishiye Milele Na Milele, Na Kwa Kupitia Mamlaka Ya Jina Lako, Ee Yesu Kristo Wa Nazareti, Mwana Wa Mungu Uliye Hai, Ninakuomba Utakaso Mbele Zako Ee Mungu Uliye Hai Milele Na Milele, Na Mbele Zako Ee Bwana Yesu Kristo Mwana Wa Mungu Uliye Hai Milele Na Milele, Na Mbele Zako Ee Roho Mtakatifu, Uliye Hai Milele Na Milele, Nami Ninaupokea Utakaso Huu Sasa, Ulioniandalia Kabla Ya Kuwekwa Misingi Ya Ulimwengu, Na Kwa Kifo Chako Ee Bwana Yesu Pale Msalabani, Ninajitakasa Sasa Na Hata Milele Kwa Utakaso Huu Kwa Damu Ya Yesu Kristo Mwana Wa Mungu, Uliye Hai Milele Na Milele, Na Kwa Utakaso Huu Kwa Neno La Mungu Uliye Hai Milele Na Milele, Na Kwa Utakaso Huu Kwa Upako Wa Roho Mtakatifu Wa Mungu Uliye Hai Milele Na Milele; Na Kwa Utakaso Huu Kwa Jina La Yesu Kristo Wa Nazareti, Mwana Wa Mungu Uliye Hai, Uishiye Milele Na Milele! Na Kwa Utakaso Huu Ninazifisha Nguvu Zote Za Kila Aina Ya Dhambi, Na Kila Aina Ya Uchungu Wa Dhambi, Na Kila Aina Ya Magonjwa, Na Kila Aina Ya Udhaifu, Na Mauti. Na Kwa Utakaso Huu Ninang’oa Kila Aina Ya Pando Lisilopandwa Na Baba, Mungu Uliye Hai, Katika Jina La Yesu Kristo Mwana Wa Mungu Uliye Hai Milele Na Milele, Amina!
1) Ninakuomba uwepo wa Roho Mtakatifu, Unisaidie Kujichunguza Na Kuiona Kila Dhambi Ndani Yangu, Na Kisha Uniwezeshe Kuishinda Aibu Na Haya Mbele Zako Na Mbele Za Wanadamu, Ili Niweze Kukiri Na Kuomba Toba Mbele Zako Ee Mungu Kikweli Kweli. Tena Ninaomba Uniwezeshe Kwa Upesi, Niamue Kikweli Kweli, Kubadilika Kwa Kutokutenda Dhambi Tena, Unisaidie Kuyaacha Maasi Yangu Yote, Ili Niwe Safi Na Niwe Tayari Wakati Wote Moyoni Mwangu, Rohoni Mwangu, Na Mwilini Mwangu; Kwa Maana Maisha Yangu Hapa Duniani Ni Kama Moshi, Kama Mvuke, Na Kama Ua Linalochanua Asubuhi Na Kisha Jioni Hunyauka. Hivyo Ninaomba Kila Saa Uniwezeshe Niwe Tayari Muda Wote, Bila Mawaa Wala Makunyanzi Yoyote Kuwa Tayari Kwa Kuingia Mbinguni. Ninaomba Unyenyekevu Wa Kweli Mbele Zako Ee, Mungu Wangu, Na Mbele Za Wanadamu. Ninaomba Unisamehe Sana Ee Baba, Ninaomba Unisamehe Sana, Ee Bwana Yesu, Ninaomba Unisamehe Sana, Ee Roho Mtakatifu. Ninaomba Unisaidie Ee, Mungu Wangu, Ninaomba Neema Yako Tele, Maana Bila Wewe Mimi Siwezi Neno Lolote.
2) Ninakusihi Ee Bwana Yesu, Uniwezeshe Kwa Ujasiri Wote Na Kutoka Ndani Kabisa Ya Moyo Wangu, Kufanya Matengenezo – Yaani, Kujichunguza Na Kufanya Marekebisho Kwa Maeneo Yale Niliyowakosea Watu Wengine. Niwezeshe Kwenda Kukiri Makosa Na Kuwaomba Msamaha, Kuwarudishia Mali Zao Nilizowadhulumu, Nilizokopa, Nilizoiba, Na Hata Niwezeshe Kulipa Gharama Pale Inaponibidi Kwa Utii Na Unyenyekevu Wote. Kwa Uhakika Kabisa Nianze Na Jirani Zangu. Nianze Kwa Mke/Mume Wangu, Mtoto/Watoto Wangu, Ndugu Zangu, Nyumbani Mwangu, Mtaani Kwetu, Kazini Kwetu, Kanisani Kwetu, Au Mtu Yeyote Yule Wa Karibu Sana Nami; Yaani Nianze Kuwa Shahidi Yerusalemu, Uyahudi, Samaria Na Hata Mwisho Wa Nchi, Sawa Na Neno Lako. Tena Ninaomba Uwape Rehema Na Neema, Na Moyo Wa Msamaha Watu Wote, Hasa Wale Niliowakosea Na Kuwakwaza, Ili Waweze Kunisamehe Na Tena Wawe Na Amani Na Wanifurahie Na Wawe Na Amani Nami; Ninaomba Sawa Na Neno Lako Katika Waebrani 12:14, Kwamba, Tutafute Kwa Bidii Kuwa Na Amani Na Watu Wote Na Huo Utakatifu, Maana Umesema Tukiyakosa Hayo Hatutakuona Wewe Ee Mungu Wetu Katika Ulimwengu Huu, Na Hata Ule Ujao! Baba Unisaidie, Ninapenda Kukuona Na Kukuabudu Wewe Peke Yako! Ninpenda Kukuona Ee Bwana Yesu, Ninapena Kukuona Ee, Roho Mtakatifu, Ninapenda Kufika Mbinguni! Ni Wewe Tu Wa Kuniokoa, Kuniponya, Na Kunitengeneza Milele!
3) Ninakuomba Baba, Unisamehe, Kwa Maana Mimi Ndiye Mkosaji, Kwa Ajili Ya Wale Ninaowafahamu Na Kuwaona Ya Kuwa Wameniudhi Na Kunikosea, Baba Ninakuomba Uniwezeshe Kuwasamehe, Nami Ninawasamehe Kabisa! Kama Ni Kweli Wao Ndio Wamenikosea Mimi. Ninaomba Nguvu Ya Kuwasamehe Kabisa Bila Kinyongo Moyoni, Na Wala Nisiuhesabu Wala Nisikumbuke Kamwe Ubaya Wao Kwangu Milele. Unisaidie Kusamehe Kwa Namna Kamili Kabisa, Kama Wewe Ulivyotusamehe Na Ulivyoagiza. Unisaidie Kuwapenda Hata Adui Zangu Wote Kwa Upendo Wako. Asante Baba! Ninaomba Uniwezeshe Kuwa Na Amani Na Watu Wote, Ile Amani Itokayo Kwako, Amani Ipitayo Kila Akili Na Ufahamu Wote. Nami Ninatangaza Msamaha Sasa Kwa Wote, Natena Nitatangasa Suluhu! Nami Ninkubali Kuupokea Msamaha Kwa Wote Sasa; Katika Jina La Yesu Kristo!
4) Ninajitakasa Kwa Damu Ya Yesu Kristo: Ninajifunika, Pamoja Na Nyumba Yangu, Familia Yangu, Kanisa Lako, Jamii Yangu, Wapendwa Wangu, Mali Zangu Zote, Taifa Langu, Na Kila Uongozi Wa Kikanisa, Kiserikali Na Kidini, Kwa Damu Ya Yesu Kristo; Sasa Na Kila Wakati Na Popote, Milele Na Milele, Amina.
5) Ninasimama Na Kuwaombea Watu Wote Toba Na Msamaha Na Utakaso Kwa Damu Yako Ee Bwana Yesu, Mbele Zako Baba, Katika Jina La Yesu Kristo Aliye Hai.
6) Ninaondoa Kila Lililo Chukizo Mbele Zako Ee Mungu Baba, Kwa Jina La Yesu Na Kwa Damu Takatifu Ya Yesu Kristo:
a) Ninayaondoa Maneno Machafu Yote!
Nikiyafuta Na Kuyaharibu Maneno Yote Mabaya Niliyowahi Kuyatamka Au Yaliyowahi Kutamkwa Dhidi Yangu, Familia Yangu, Kanisa Lako, Jamii Yangu, Na Taifa Langu, Hata Pia Kizazi Chote Katika Ulimwengu Huu; Ambayo Shetani Anayatumia Dhidi Yangu, Nyumba Yangu, Kanisa Lako, Taifa Langu, Na Kizazi Chote. Ninaungama Na Kutubu Na Kuyafuta, Maneno Hayo Popote Yalipo. Ardhini, Baharini, Angani, Mwezini, Kwenye Nyota Au Kwenye Jua; Kwa Jina La Yesu. Ninaugeuza Ukiri Wangu Mbaya Na Ulio Kinyume Na Maagizo Ya Mungu Ili Uwe Ukiri Mwema Kwa Utukufu Wa Mungu Mwenyezi. Ninatumia Damu Ya Yesu, Kuyafuta Maneno Ya Ukiri Mbaya Na Wa Kinyume Katika Jina La Yesu Kristo Aliye Hai, Amina!
b) Ninaziondoa Mali Zote Za Mashetani, Mapepo Na Majini Katika Kila Eneo La Maisha Yetu:
Katika Jina La Bwana Wetu Yesu Kristo Wa Nazarethi, Ninaharibu Kila Kitu Nilicho Nacho Ambacho Ni Mali Ya Shetani, Ninakiharibu Kila Kilicho Cha Shetani, Na Vitu Vyote Vyenye Uhusiano Na Shetani, Vyenye Nguvu Za Shetani Ambavyo Nimevinunua Kwa Fedha Zangu Au Kupewa Kama Zawadi, Na Kila Mahali Ninapopakanyaga Au Kukaa Na Kuishi. Ninazitakasa Nguo Zangu Zote, Mavazi, Mapambo, Urembo, Manukato, Mafuta Na Vipodozi Vyote; Kwa Damu Ya Yesu Kristo Wa Nazarethi. Pia Ninaharibu Kila Kitu Na Mahali Popote Katika Ulimwengu Wa Kiroho Na Kimwili, Penye Mfano Wangu, Mali Zangu, Fedha Zangu, Jina Langu, Sehemu Yoyote Ya Mwili Wangu, Kucha, Nywele Zangu Na Yoyote Yanayotokana Na Hayo Ambavyo Viko Baharini, Angani, Duniani, Kwenye Matumizi Ya Mahekalu Ya Sanamu Au Madhabahu Za Shetani, Ninaamuru Moto Wa Roho Mtakatifu Kuwaunguza Wajumbe Wote Wa Shetani Wanaofanya Vitu Vyo Vyote Dhidi Yangu, Kanisa, Taifa, Na Dhidi Ya Jamii Yangu Kwa Damu Ya Yesu Kristo Wa Nazarethi.
c) Ninaviondoa Vifungo Vyote (Katika Moyo Nafsi Na Mawazo)
Katika Jina La Yesu Kristo Wa Nazarethi, Baba Wa Mbinguni, Ninakuinulia Mkono Wangu Wa Kuume Mimi Mwanao/ Binti Yako … (Taja Jina Lako) Nitazame Bwana Maana Nguvu Na Uwezo Wote Unatoka Kwenye Kiti Chako Cha Enzi Kama Ilivyoandikwa Katika Zabauri 52:11-12. Kusema ''Mara Moja Amenena Mungu Mara Mbili Nimeyasikia Haya, Ya Kwamba Nguvu Zina Mungu Na Fadhili Ziko Kwako Ee Bwana, Maana Ndiwe Umlipaye Kila Mtu Sawa Sawa Na Haki Yake. Baba Wa Mbinguni , Ninapokea Nguvu Kutoka Kwako Sasa Katika Jina La Yesu. Ninatumia Nguvu Hizi Kufuta, Kuvunja, Kuharibu Na Kujitenga Mwenyewe Kutoka Kwenye Laana Zote Na Maagano Yote Yaliyofanywa Dhidi Yangu. Ninaamuru Laana Zote Pamoja Na Mapatano Na Mazindiko Yaliyofichwa Popote Dhidi Ya Maisha Yangu, Kujidhihirisha Sasa Katika Jina La Yesu. Ninaamuru Moto Wa Roho Mtakatifu Na Damu Ya Yesu Kuwadhihirisha Majeshi Ya Pepo Wabaya, Majini, Mashetani, Na Maadui Zangu Wote. Ninaziharibu Nguvu Zote Za Giza Na Za Mapepo Katika Jina La Yesu Kristo-Amen
d) Ninaziondoa Dhambi Zote Za Mababu:
Baba Wa Mbinguni Ninaleta Dhambi Zote Za Mababu Zangu Mbele Zako. Ninazitubu Na Kuziungama Dhambi Zao Zote, Kwa Maana Walikutenda Dhambi, Na Ya Kuwa Zimekuwa Pando Usilolipanda Baba, Shina La Uchungu Limealo Na Kuleta Mabaya Kwa Wengi, Na Hata Kwa Kizazi Na Kizazi Na Kwa Wote Leo Hii. Ninaziungama Dhambi Zao Zote Za Chuki, Hasira, Kuuwa Binadamu Wenzao, Kuabudu Sanamu, Kuwauza Na Kuwanunua Wanadamu, Kutoa Kafara Za Damu Za Watu Kwa Miungu Na Kwa Sanamu, Kula Nyama Za Watu Na Kila Matendo Mengine Ya Kishetani Walioyafanya. Baba Pia Ninaungama Dhambi Za Wazazi Wangu Na Uovu Wao Walioutenda Mbele Zako. Baba Ninakusihi Uwe Na Rehema Katika Jina La Yesu Kristo, Ninawasamehe Makosa Yote Waliyonitendea Katika Jina La Yesu. Ninaomba Uzisahau Dhambi Na Makosa Na Uovu Wao Wote. Kwa Hiyo Ninajitenga Na Kuwatenga Wote Wa Leo Kutoka Kwenye Adhabu Ya Makosa Hayo, Katika Jina La Yesu.
e) Ninaziondoa Dhambi Na Laana Za Wahenga (Wakale)Katika Jina Lenye Nguvu Na UwezaLaBwana Wetu Yesu Kristo Wa Nazarethi; Ninazitubu Dhambi Zilizofanywa Na Hao Wazee Wetu Wa Kale (Wahenga) Ambazo Kwa Hizo Laana Imenipata Na Kuniandama Hata Leo Hii, Mimi Na Uzao Wangu. Ninazivunja Na Kuziharibu Laana Zote Zilizosababishwa Na Uovu Wowote Walioufanya; Ninaziharibu Kwa Jina La Yesu Kristo Wa Nazarethi, Laana Zote, Mapatano Na Matambiko Katika Upande Wa Baba Yangu Na Mama Yangu, Baba Mkwe Na Mama Mkwe Wangu Na Ndugu Zangu Wote; Ninaziharibu Na Kuzivunja Katika Jina La Yesu. Bila Kujali Ni Aina Gani Ya Laana Iliyowekwa Juu Yangu; Bila Kujali Ni Maagano Gani Wahenga Wangu Wamefanya Na Shetani; Na Bila Kujali Ni Wapi Wamefanya Mambo Ya Matambiko, Mazindiko Juu Yangu, Iwe Angani, Ardhini, Baharini, Ninayaharibu Yote Katika Jina La Yesu, Amina. Pia Ninazivunja Laana, Maagano Na Matambiko, Niliyofanyiwa Na Baba Yangu Na Mama Yangu Na Wakwe Zangu, Pamoja Na Wazazi Wao (Babu Na Bibi) Kutoka Kizazi Chochote Kwa Upande Wa Baba Yangu Na Mama Yangu, Na Wakwe Zangu, Bila Kujali Laana, Matambiko, Mazindiko, Mapatano Na Ushirikina Na Ushirikiano Uwao Wote Yalifanyika Wapi. Ninaamuru Yote Kuvunjika Na Kuharibiwa Katika Jina La Yesu Kristo, Amina.
f) Ninaziondoa Dhambi Na Laana Zote Kutoka Kwangu Mwenyewe,
Katika Jina La Yesu Kiristo, Ninakwenda Kinyume Na Laana Zote Nilizozisababisha Mimi Mwenyewe, Juu Ya Maendeleo Yangu Na Maisha Yangu, Kwa Kujua Na Kutokujua. Ninakuondoa Wewe Dhambi Na Uchungu Wako, Na Ninakuvunja Wewe Laana Popote Pale Ulipojificha, Katika Roho Yangu, Katika Mwili Wangu, Katika Nafsi Yangu, Angani Duniani Na Baharini, Ninakuharibu Na Kuzivunja Nguvu Zako Zote Katika Jina La Yesu. Ninakuja Kinyume Cha Maagano Niliyoyafanya Kwa Uchawi, Ushirikina Na Kwa Namna Yoyote Ile, Na Miungu Ya Sanamu, Pepo Wachafu, Maruahani, Majini Bahari, Waume Wa Kipepo, Wake Wa Kipepo, Watoto Wa Kipepo, Familia Za Kipepo Na Mizimu N.K Katika Jina La Yesu, Mazindiko Yote Niliyojifanyia, Ninayaharibu Yote. Ninajiondoa Katika Mazindiko Hayo. Ninalifuta Jina Langu Kwenye Kitabu Cha Shetani Na Kumbukumbu Zake Zote, Na Katika Kitabu Cha Mauti Na Kuzimu. Ninajitangazia Uhuru Sasa, Katika Jina La Yesu Amen. Ninajifunika Kwa Damu Ya Yesu Kristo Wa Nazarethi, Mwana Wa Mungu Aliye Hai. Amina!
g) Ninaziondoa Dhambi Na Laana Zote, Kutokana Na Kuto Mtii Kwangu Mungu Ninaziungama Na Kuzitubu Dhambi Zangu Zote; Kutokutoa Zaka(Fungu La Kumi), Kutokutimia Ahadi Na Nadhiri Nilizoahidi Mbele Za Mungu, Kusema Maneno Mabaya Juu Wa Watumishi Wa Mungu Na Waliookoka, Uzushi, Hisia Mbaya Na Dhamiri Mbaya Kwa Watu, Kutokuwatunza Wa Nyumbani Mwangu, Kutowajali Yatima Na Wajane, N.K. Kwa Jina Lako Baba, Katika Jina La Yesu, Ziondoe Laana (Malaki 3: 8-12) Parare, Nzige, Tunutu Na Viwavi Kutoka Kwangu. Ninyeshee Mvua Za Mwanzo Na Za Mwisho. Nijaze Tena Baraka Zako, Katika Jina La Yesu, Amen.
h) Ninaiondoa Kutoka Kwa Shetani Na Wajumbe Wake, Mikataba, Uharibifu, Laana, Na Utumishi Wote.
Katika Jina La Yesu Ninavunja Na Kuzimisha Laana Zote. Maagano Na Mazindiko Ya Shetani Na Wajumbe Wake Walio Dhidi Yangu. Ninaharibu Uchawi, Laana, Na Maagano Kutoka Kwa Miungu Yote Ya Uongo, Wachawi Waganga Wa Kienyeji, Na Majini Ya Bahari, Mizimu, Waume Au Wake Wa Kipepo, Watoto Wa Kipepo, Makazi Ya Kipepo, Mali Za Kipepo, Kutoa Mimba, Kujichua, Kukosa Nguvu Za Kiume/Kike, Utasa, Ugumba, Kutiwa Maji, Mikutano Ya Wachawi, Mahekalu Ya Kipepo, Kutoka Angani, Nchi Kavu Na Baharini (Hes.22). Ninaamuru Moto Wa Roho Mtakatifu Kuteketeza Na Kuiharibu Mipango Yote Iliyopangwa Dhidi Yangu, Katika Jina La Yesu Kristo Wa Nazarethi, Amen.
i) Ninaiondoa Dhambi Na Laana Ya Nchi
Katika Jina La Bwana Wetu Yesu Kristo Wa Nazarethi Ninaiondoa Dhambi Na Laana Ya Nchi Yangu, Mji Wangu, Na Kijiji Changu Ninavunja Laana Zote, Matambiko Maagano Na Mazindiko Yaliyofanywa Dhidi Ya Watu Wote, Wenye Mamlaka, Wakuu Wa Serikali, Vyama, Vyombo Vya Ulinzi Na Usalama Na Vyombo Vya Habari Na Mawasiliano; Na Ninaharibu Nguvu Zote Zilizofanyika Dhidi Yao, Katika Jina La Yesu Kristo. Ninaivunja Laana Ya Mauti, Kichaa, Tamaa, Umaskini, Masongwa, Kutaka Kujua(Udadisi), Kuvunjika Kwa Ndoa, Utasa, Kutokuoa, Au Kutokuolewa, Ushirikina, Udini, Udhehebu, Imani Potofu, Ujinga, Dhuluma, Wizi, Ujambazi, Rushwa, Ubakaji, Matusi, Magomvi, Mapigano, Migomo Makazini, Shuleni, Mitaani, Na Katika Vyombo Vya Dola! Kunyanyaswa, Kuonewa, Kukata/Kujikata Viungo Vya Mwili, Imani Potofu, Kutaka Kujiua, Vita Na Umwagaji Wa Damu Isiyo Na Hatia(Mauti), Uchafu Na Ufisadi Wote, N.K. Ninajitenga Sasa Kutoka Kwenye Laana Hizo Zote, Maagizo Na Mazindiko Katika Jina La Yesu, Amen. Ninaharibu Nguvu Zote Na Mipango Ya Wachawi, Washirikina, Miungu Ya Uongo, Miti Mibaya, Mto, Mapori Mabaya N.K Katika Taifa Langu, Wenye Mamlaka Na Viongozi Wa Kiserikali, Viongozi Wa Kimila Na Kidini, Mji Wangu Na Kijiji Changu. Ninaamuru Moto Wa Roho Mtakatifu Kuviharibu Vyote Katika Jina La Yesu, Amen.
j) Ninaondoa Kila Aina Ya Mapatano Na Makubaliano
Ninavunja Maagano Na Mazindiko Yaliyofanywa Kwa Ajili Yangu, Nchini Na Baharini Pia Ninaharibu Maagano Na Mazindiko Yaliyofanywa Kwa Niaba Yangu Kwa Miungu Ya Uongo, Miti, Mivinjo (Shrine) Mito Na Vijito.(Ninafunga Na Kuharibu Mito Yote Mibaya, Miungu Ya Uongo, Vijito Na Wachawi) Katika Kijiji Changu Au Mji Wangu, Ninajitenganisha Sasa Kutoka Kwenye Laana Hizo, Maagano Na Mazindiko Katika Jina La Yesu, Amen.
k) Ninayaondoa Mashambulizi Ya Waziwazi Na Ya Ndoto
Katika Jina La Yesu Wa Nazarethi Ninavunja Nguvu Zote Za Giza Dhidi Yangu Zinazokuja Waziwazi Na Ndotoni. Ninayafunga Na Kuyatupa Mapepo Yote Yanayonishambulia Waziwazi Na Kwa Njia Ya Ndoto. Ninakuja Kinyume Na Ndoto Zote Za Kipepo Dhidi Ya Maisha Yangu. Ninawakemea, Ninafunga Na Kuyaharibu Mapepo Yote Yanayonipa Na Kuwapa Watu Chakula Kwenye Ndoto, Wanawake Na Wanaume Wa Kipepo Wanaokuja Ili Kufanya Mapenzi Nami Au Na Watu Wengine Katika Ndoto, Mahoka Yote, Yanayokuja Katika Ndoto, Mapepo Yote Yanayofanya Kuogelea Kwenye Mto, Mapepo Yote Ya Kuoana Nami Au Watu Katika Ndoto,(Majinamizi). Ninaamuru Moto Wa Roho Mtakatifu Kuwateketeza Wote Katika Jina La Yesu, Amina. Katika Jina La Yesu Kristo Wa Nazarethi, Ninazivunja Kazi Na Nguvu Za Roho Zozote Chafu Juu Yangu, Roho Ya Kiburi, Hasira, Uchungu, Kukataliwa, Makosa, Uasi, Uvivu, Chuki, Mashaka, Kuchanganyikiwa, Kujidharau, Kutokuamini, Anasa, Ukaidi, Mashindano, Mateso, Umaskini, Ukosefu Wa Usingizi, Mauti, Uoga, Uongo, Kutokusamehe, Uasherati, Uzinzi, Uchafu, Kutokutii, Wivu, Uuwaji, Ulevi, Ujinga, Usahaulifu, Bumbuwazi, Matusi, Kutokujali Na Kupuuzia Mambo Ya Mungu, N.K Ambao Zinanikandamiza Roho Yangu, Nafsi Yangu, Moyo Wangu, Mawazo Yangu Na Hali Ya Mazingira Yangu. Ninazikemea Na Kuzifunga, Na Kuzitoa Nje Roho Hizo Kwa Jina Ka Yesu. Ninaamuru Moto Wa Roho Mtakatifu Kuwateketeza Wote Popote Pale Mlipojificha, Angani, Nchini Na Baharini. Ninatumia Damu Ya Yesu Kristo Ya Agano La Milele, Kujifunika Milele Ili Msiweze Kurudi Tena Kwangu Milele, Katika Jina La Yesu, Amen.
l) Ninaziondoa Sherehe Za Miji Na Mila Za Kifamilia
Katika Jina La Yesu Kristo Ninazikemea Na Kuziharibu Mila Zote Za Kipepo Sherehe Na Matukio Yanayotendeka Na Jamii Yangu Au Mji Wangu. Ninayaharibu Mapepo Yote Yanayoabudiwa Katika Sherehe Hizo, Ninatumia Damu Ya Yesu Kutangaza Vita Na Ushihi Wa Milele Dhidi Yenu Katika Jina La Yesu. (Kumbuka, Ujiepushe Kushiriki Sherehe Hizo Maana Kwa Kufanya Hivyo Utakuwa Unayapendeza Mapepo Hayo Na Kuyaabudu.)
m) Ninajitenga Kabisa Mwenyewe Na Laana, Maagano, Mikataba, Ushirikina Na Mazindiko Yote:
Baba Wa Mbinguni, Ninajishusha Na Kujitenganisha Na Laana Zote, Maagano, Mazindiko N.K Niliyofanyiwa; Mimi Niko Huru Sasa, Hivyo Ninayo Haki Ya Kuchagua Nitakayemtumikia. Ninachagua Kumtumikia Baba Wa Mbinguni, Yesu Kristo Na Roho Mtakatifu; Milele! Mimi Ni Kiumbe Kipya Na Ni Mpya Kila Siku Ya Maisha Yangu. Roho Mtakatifu Yu Juu Yangu Sasa. Ninayaweza Mambo Yote Katika Yesu Kristo Anitiaye Nguvu (Fil 4:13) Neno La Mungu Linasema Kwa Maneno Yako Utahesabiwa Haki Na Kwa Maneno Yako Utahukumiwa. (Mathayo. 12:37) Baba Nifanye Kuwa Na Haki Kwa Maneno Ya Kinywa Changu Kwa Kuwa Uzima Na Mauti Vimo Katika Uwezo Wa Ulimi (Mithali 10:21). Basi Mwana Akiwaweka Huru, Mtakuwa Huru Kwelikweli (Yohana. 8:36) Kamwe Sitateswa Tena Na Shetani Pamoja Na Wajumbe Wake Kwa Maana Mimi Tayari Niko Huru, Katika Jina La Yesu Kristo. Amen.
n) Ninajifungua Na Ninajiweka Huru Sasa Na Hata Milele!
Katika Jina La Yesu, Ninavunja Nguvu Zote Za Giza Zilizonifunga. Ninajiweka Huru Kutoka Kwenye Nguvu Za Giza Dhidi Yangu. Ninajiweka Huru Kutoka Kwenye Vifungo Vya Uchawi, Waume Wa Kipepo, Wake Wa Kipepo, Watoto Wa Kipepo, Makazi Ya Kipepo, Mali Za Kipepo, Mapepo Ya Kurithi, Majini Bahari, Maruhani, Misukule Na Mizimu, Subiani, Maruani, Zakuani, Makata, Ulemavu, Ajali, Mikosi, Laana, Umasikini, Magonjwa Yote! N.K. Sikiliza Enyi Nguvu Za Giza, Imeandikwa Katika Kitabu Cha Matayo 18:18 Kusema, Amini Nawaambia Yoyote Mtakayoyafunga Duniani Yatakuwa Yamefungwa Mbinguni Na Yoyote Mtakayo Yafungua Duniani Yatakuwa Yamefunguliwa Mbinguni. Ninasimama Juu Ya Neno Hili Na Kujifungua Kutoka Kwenye Aina Zote Za Giza Na Nguvu Zote Za Kipepo Katika Jina La Yesu, Amen!
2. Ninazivaa Silaha Za Mungu Na Mamlaka Ya Kimungu, Sasa Na Hata Milele, Kwa Jina La Yesu.
a. Ninakiri Neno Lako Hili Ee, Mungu.
1) Imeandikwa Katika Matayo 16:19, Nitakupa Wewe Funguo Za Ufalme Wa Mbinguni Na Lolote Utakalo Lifunga Duniani Litakuwa Limefungwa Mbinguni Na Lolote Utakalo Lifungua Duniani Litakuwa Limefunguliwa Mbinguni.
Baba Sasa Ninazipokea Funguo Zote Za Ufalme Wa Mbinguni Ili Kufungua Milango Ya Mambo Yasiyowezekana Chochote Nitakacho, Nitakacho Kifungua Sasa Kitafunguka Milele Katika Jina La Yesu, Amen.
2) Imeandikwa Katika Wafilipi 4:13 - Nayaweza Mambo Yote Katika Yesu Kristo Anitiaye Nguvu. Katika Jina La Yesu, Amen.
3) Imeandikwa Katika Luka 1:37, - Kwamba Hakuna Neno Lisilowezekana Kwa Mungu.
Baba Upo Pamoja Nami Sasa Na Hakutakuwa Na Chochote Ambacho Hakitawezekana Kwangu Katika Jina La Yesu-Ameni.
4) Imeandikwa Katika Zekaria 4:6, ''Si Kwa Uwezo Wala Si Kwa Nguvu Bali Ni Kwa Roho Yangu Asema Bwana Wa Majeshi''
Baba Vita Si Vya Kwangu Bali Ni Kwa Roho Yako Utanipigania Katika Jina La Yesu-Amen!
5) Katika Isaya 41:10, Imeandikwa, Usiogope Kwa Maana Mimi Ni Pamoja Nawe, Usifadhaike Kwa Maana Mimi Ni Mungu Wako, Nitakutia Nguvu, Naam Nitakushika Kwa Mkono Wa Kuume Wa Haki Yangu.
Baba Ninakushukuru Kwa Kuwa Upo Pamoja Nami Kwa Ajili Ya Kunitia Nguvu, Kunisaidia, Kunishika Na Kuwa Mungu Wangu, Moyo Wangu Umetiwa Nguvu, Katika Vita Hii Katika Jina La Yesu, Amen!
6) Imeandikwa Katika Zaburu 105: 15, , Msiwaguse Masikini Wangu Wala Msiwadhuru ''Masihi Wangu''
Nimefunikwa Kwa Damu Ya Yesu Kristo Na Upako Wa Roho Mtakatifu, Shetani Huwezi Kunigusa Kwa Sababu Mimi Ni Mpakwa Mafuta Na Nabii Wa Mungu, Maisha Yangu Yako Mikononi Mwa Yesu Kristo Na Ninayo Chapa Yake. Nimetiwa Muhuri Wa Roho Mtakatifu Usinitaabishe Tena, Katika Jina La Yesu Amen!
7) Katika Isaya 54:17, Imeandikwa, Kila Silaha Itakayo Fanyika Juu Yako Haitafanikiwa Na Kila Ulimi Utakaoinuka Juu Yako Katika Hukumu Utauhukumu Kuwa Mkosa. Huu Ndio Urithi Wa Watumishi Wa Bwana Na Haki Yao Inayotoka Kwangu Mimi, Asema Bwana.
Katika Jina La Yesu Ninaharibu Kila Silaha Ya Shetani Iliyofanywa Dhidi Yangu, Silaha Ya Kiroho Au Ya Kimwili Ninaulaani Na Kuufunga Kila Ulimi Utakaoinuka Dhidi Yangu Katika Hukumu, Kwa Kuwa Huu Ni Urithi Wangu Kama Mtumishi Wa Mungu, Ni Haki Yangu Kwa Bwana.
3. Ninakualika Na Uwepo Wako Na Nguvu Zako, Ee, Mungu.
Katika Jina Kuu Linalotikisa Falme Na Mamlaka La Bwana Wetu Yesu Kristo Wa Nazareth, Katika Jina Litendalo Maajabu La Bwana Wetu Yesu Kristo Wa Nazarethi, Baba Wa Mbinguni; Ninaita Uwepo Wako Mahali Hapa, Ninaita Uwepo Wa Bwana Yesu Kristo Wa Nazareti. Asante Mungu Yesu Kristo Na Roho Mtakatifu Kuniunga Mkono Katika Vita Hivi Katika Jina La Yesu Kristo Amen.
i) Ninakualika Roho Mtakatifu Ukae Ndani Yangu Nami Ndani Yako, Unijaze Na Kunitumia Upendavyo.
Roho Mtakatifu Ninaomba Uwe Pamoja Nami Katika Vita Dhidi Ya Shetani Na Wajumbe Wake. Roho Mtakatifu Wewe Ni Mfariji Wangu. Pigana Vita Hivi Kwa Ajili Yangu Na Unifariji Katika Jina La Yesu. Siwezi Kuomba Kama Vile Uombavyo Wewe. Nakusihi Sema Sasa Ukitumie Kinywa Changu Katika Jina La Yesu. Ninakuomba Uweke Mamlaka Na Uweza Wako Katika Moyowangu Na Kinywa Changu. Roho Mtakatifu Uniongoze Na Unilinde, Unifundishe Jinsi Ya Kuomba Nitumie Kama Shoka Lako Katika Vita Hivi, Dhidi Ya Shetani Na Wajumbe Wake. Roho Mtakatifu Wewe Ni Mfariji Wangu. Pigana Vita Hivi Kwa Ajili Yangu Na Unifariji Katika Jina La Yesu Siwezi Kuomba Kama Vile Uombavyo Wewe. Nakusihi Sema Sasa Ukitumia Kinywa Changu Katika Jina La Yesu. Roho Mtakatifu Uniongoze Na Unilinde, Unifundishe Jinsi Ya Kuomba, Kuzungumza Vizuri Na Watu, Kushuhudia, Kufundisha Neno La Mungu Na Katika Kuhubiri Neno La Mungu; Na Katika Kukemea Kwa Mamlaka Kila Kazi Na Na Nguvu Za Shetani Na Pepo Wabaya Na Watu Waovu; Unitumie Kama Shoka Lako Katika Vita Hivi Vya Adui. Uje Kwangu Na Kwa Kanisa Lako Katika Nguvu Na Uweza Wako Na Ukaonyeshe Ukuu Wako Dhidi Ya Shetani Na Wajumbe Wake, Ili Wote Wahame Na Kuacha Huru Tukimuabudu Mungu Baba, Mungu Mwana, Na Wewe Ee, Mungu Roho Mtakatifu; Simama Sasa Tamalaki Sasa Na Utende Kwa Nguvu Za Uweza Wako; Ni Katika Jina La Yesu Kristo Wa Nazareth, Amen.
ii) Ninaviruhusu Vikosi Vya Majeshi Ya Malaika Watakatifu Wa Mungu Aliye Hai Milele Na Milele; Wawe Katika Vita Upande Wangu.
Katika Jina Lenye Nguvu La Bwana Wetu Yesu Kristo Wa Nazarethi. Ninyaruhusu Na Kuyaamuru Majeshi Ya Malaika Wa Vita Kutoka Ufalme Wa Mungu; Ninawaamuru Enyi Malaika Wote Kukaa Kwenye Nafasi Zenu Dhidi Ya Shetani Na Mapepo Yote, Sambaeni Kila Mahali Sasa, Mjieneze Katika Anga, Nchi Na Bahari, Na Muangamize Nguvu Zote Za Giza Katika Anga, Nchi Kavu Na Baharini Mpigeni Shetani, Majini, Wachawi Na Majeshi Ya Pepo Wabaya Bila Kukoma, Haribuni Mipango Yote Waliyoifanya Dhidi Yangu, Familia Yangu, Taifa Langu, Jamii Yangu, Kanisa La Mungu Na Watu Wote. Ninawamuru Enyi Malaika Na Bwana Mnizunguke Kama Wigo Sasa Na Milele. Mnizunguke Mimi, Familia Yangu, Jamii Yangu, Taifa Langu, Kizazi Hiki, Na Kanisa La Mungu Aliye Hai; Katika Jina La Yesu Kristo-Amen.
iii) Ninaialika Damu Ya Yesu Kristo
Ninajifunika Kwa Damu Ya Yesu Kristo. Ninawaloweka Watu Wa Familia Yangu, Ndugu Zangu, Nyumba Yangu, Ofisi Yangu, Chakula Changu, Fedha Zangu, Kiwanja Changu, Rafiki Zangu, Majirani Zangu, N.K Katika Damu Yenye Nguvu Ya Yesu Kristo Wa Nazareth. Ninalifunika Anga Lote, Nchi Yote Na Bahari Yote Kwa Damu Ya Yesu Kristo; Shetani Imeandikwa Katika Ufunuo 12: 11 ''Nao Wakamshinda Shetani Kwa Damu Ya Mwanakondoo Na Kwa Neno La Ushuhuda Wao '' Nimetumia Damu Ya Yesu Kukushinda Sasa Na Hata Milele Katika Jina La Yesu!
4. Ninamshughulikia Shetani, Kazi Zake, Na Majeshi Yake Yote.
a. Ninazifunga, Kuziharibu, Na Kuutupilia Kuzimu Ulinzi Wote Wa Kipepo
Ninayafunga Kwa Minyororo Na Kuyatupa Katika Shimo La Giza Mapepo Ya Ulinzi Yanayolinda Laana Za Maagano, Mazindiko, Uchawi Ushirikina Na Mahirizi, Udhaifu, Magonjwa, Uchungu, Huzuni, Mashaka, Kutokuamini, Upumbavu, Ujinga, Kuchanganyikiwa, Ukichaa, Uharibifu, Tamaa, Hisia Mbaya, N.K Dhidi Ya Maisha Yangu Kanisa La Mungu, Taifa Langu, Ukoo, Jamii Mtaani Kwangu N.K.. Ninaziharibu Hati Za Makubaliano, Mashitaaka, Na Ninawafunga Wote Katika Giza La Milele. Ninaamuru Moto Wa Roho Mtakatifu Kuwatesa Mchana Na Usiku Katika Jina La Yesu, Pale Yatapojaribu Kunigusa, Kumgusa Yeyote, Na Kugusa Chochote Katika Maisha Yetu. Ninaitumia Damu Ya Yesu Kuziba Nafasi Mlizokuwa Mmekalia, Katika Roho, Mwili, Nafsi, Angani, Ardhini, Baharini, Katika Mito, Katika Uongozi Serikalini, Mashuleni, Vyombo Vya Dola, Makazini, Mahospitalini Na Vituo Vya Afya, Makanisani, Misikitini Na Majumbani; Katika Wanyama, Vitu, Sanamu, Midoli, Milimani, Misituni N.K. Kwa Jina La Yesu Mwana Wa Mungu Aliya Hai!, Amen.
b. Ninayafunga, Ninayaharibu, Na Kuyatupilia Kuzimu; Mapepo Yote Yanayopinga Na Kuzuia Maombi, Kusifu Na Kuabudu Makanisani Na Katika Maisha Ya Watu Wa Mungu.
Katika Jina La Bwana Wangu Yesu Kristo; Ninakemea, Ninafunga Na Kuyaangamiza Mapepo Yote Yanayozuia Maombi Na Majibu Ya Maombi – Katika Ulimwengu Wa Kiroho Na Kimwili, Angani, Katika Nchi Na Baharini. Pia Ninamharibu Kila Pepo Anayeninginia, Kila Pepo Arukaye Na Wale Walionyimwa Chakula. Ninawatupa Hadi Kuzimu Katika Jina La Yesu. Ninaviharibu Vipingamizi Vyenu Vyote Vya Maombi Na Majibu Ya Maombi Yangu Na Ya Kanisa, Ninawatupa Katika Giza La Milele. Ninawafungia Huko Hata Siku Ya Bwana Ya Hukumu. Pia Ninayakemea, Na Kuyafunga Na Kuyaharibu Mapepo Yote Yanayozuia Ukombozi Wangu, Familia, Kizazi Hiki, Taifa, Kanisa, Mafanikio Yangu Na Miujiza. Ninaziharibu Kazi Zenu Dhidi Ya Maisha Yangu, Ninawatupa Wote Katika Giza La Milele Na Kamwe Msiweze Kuinuka Tena Hata Siku Ya Hukumu Ya Bwana. Ninawatumia Moto Wa Roho Mtakatifu Na Damu Ya Yesu Kuwateketeza Wote Katika Jina La Yesu Kristo, Amen.
c. Ninauondoa Ukungu Wa Kipepo
Ninatumia Moto Wa Roho Mtakatifu Na Damu Ya Yesu Kuharibu Ukungu Wa Kipepo Unaofunika Anga, Ardhi, Ndani Ya Kanisa, Katika Roho, Katika Nafsi, Na Katika Miili. Ninaharibu Kila Mfuniko Ambao, Umenifunika Na Kulifunika Kanisa Na Taifa, Na Kizazi Hiki, Katika Jina La Yesu Kristo, Amen. Ninaharibu Kila Kifuniko, Minyororo, Mafundo Na Uchawi Dhidi Yangu. Ninauamuru Moto Wa Roho Mtakatifu Kuviteketeza Vyote Na Kuvifanya Majivu Kabisa. Ninauzimisha Moshi Wa Shetani Kwangu, Dhidi Ya Maombi Yangu. Ninatumia Damu Ya Yesu Kuviharibu Vyote, Katika Jina La Yesu, Amen. Shetani, Imeandikwa Katika Kitabu Cha Luka 1:13 Kusema ''Hakuna Lisilo Wezekana Kwa Mungu.
Mikanda
Ambavyo Shetani Ameitega Dhidi Yangu Na Kanisa La Mungu. Ninayakemea
Ninayavunja Na Kuyaamuru Mapepo Yote Ya Angani Na Duniani Yapate
Kuniachia Na Kuliachilia Kanisa Kwa Jina La Yesu. Amen. Ninaamuru Moto
Wa Roho Mtakatifu Kuwateketeza Wote. Ninafunga Wote Kwa
Ufunguo Wa Hukumu Na Msiinuke Kamwe Hadi Siku Ya Bwana Ya Hukumu.
Nisikilize Sana Shetani Imeandikwa Katika Isaya 54:17 Kwamba Hakuna
Silaha Itakayofanyika Dhidi Yangu Ambayo Itafanikiwa, Na Kila
Ulinzi Utakaoinuka Juu Yangu Nitauhukumu Kwa Makosa. Ninasimama Juu
Ya Neno Hili Na Ninazilaani Silaha Zako Zote Ulizozifanya Dhidi Yangu,
Nitaziharibu Kwa Jina La Yesu, Amen!
e. Ninaifunga Mitandao Mingine Yote Ya Kipepo
Ninakufunga Shetani Na Kazi Zako Zote Kwa Jina La Yesu
Ninakukemea Shetani, Ninakwenda Kinyume Chako Kwa Damu Ya Yesu Na Kwa Moto Wa Roho Mtakatifu. Shetani Nimekushinda. Ninaukanyanga Ufalme Wako. Ninakunyanganya Kila Kilicho Changu. Ninakuamuru Kuviacha Vitu Vyangu Milele, Katika Jina La Yesu. Mimi Ni Balozi Wa Bwana, Mimi Ni Masihi Wa Bwana Yesu Kristo Amenipa Nguvu, Mamlaka Na Uwezo Wa Kuzikanyaga Nguvu, Mamlaka Na Uwezo Wako Wote Shetani, Wala Hakuna Kitakacho Nidhuru. Kumbuka Imeandikwa Katika Zaburi 105:15 Kusema Usimguse Masihi Wangu Na Wala Usimdhuru Nabii Wangu; Malaika Wa Bwana Wananizunguka Damu Ya Yesu Imenifunika Na Imo Ndani Yangu, Roho Mtakatifu Yu Ndani Yangu Na Amenipaka Mapaka Mafuta, Hivyo Ninao Upako Wa Roho Mtakatifu; Hakuna Silaha Yako Yoyote Wala Ya Majeshi Yako Ya Pepo Wabaya, Wajumbe Wa Giza Au Hata Ya Uharibifu Wako; Itakayofanyika Juu Yangu Itakayofanikiwa. Na Kila Ulimi Utakaoinuka Juu Yangu Katika Hukumu, Ninauhukumukua Ni Mkosa, Kwa Jina La Yesu Utelete! Nisikilize Shetani, Mimi Ni Kapteni Wa Jeshi La Bwana Ninasikiliza Amri Kutoka Kwa Amiri Jeshi Wangu Tu Yesu Kristo Wa Nazareti, Ambaye Vyote Viliumbwa Kwa Yeye, Ninakuamuru Uhame Katika Jina Lipitalo Majina Yote, Yesu Kristo Wa Nazareti Popote Pale Unapojificha, Ninaamuru Moto Wa Roho Mtakatifu Ukuunguze Usiku Na Mchana Hata Milele. Amina!
f. Ninazifunga Falme Na Mamlaka , Wakuu Wa Giza/Anga, Majeshi Ya Pepo, N.K.
Ninazikemea, Ninazifunga Na Kuziharibu Falme Na Mamlaka Ya Wakuu Wa Giza Hili, Majeshi Ya Pepo Wabaya Katika Ulimwengu Wa Roho. Ninaamuru Moto Wa Roho Mtakatifu Kuwateketeza Wote, Katika Jina La Yesu. Ninawagonga Wachawi Wote, Majini, Mizimu, Majini-Baharini, Wakuu Wa Giza, Roho Wa Udhaifu Na Roho Chafu Zote Zilizo Dhidi Ya Maisha Yangu Na Maendeleo Yangu Na Dhidi Ya Kanisa La Mungu, Na Taifa Zima. Ninayaaharibu Maficho Yako Na Kila Mbinu Unayoitumia Kujihami Na Kwa Moto Wa Roho Mtakatifu Ninawateketeza Wote Katika Jina La Yesu. Ninawatupa Wote Kuzimu Ninawafungia Katika Giza Milele Ninawafungia Wote Hata Siku Ya Hukumu Ya Bwana Na Wala Msiinuke Tena, Katika Jina La Yesu, Amen.
5. Ninazifunga Nguvu Za Dhambi Zote Za Kuambukiza.
6. Ninazitakasa Kwa Damu Ya Yesu Madhabahu Zote Za Ibada, (Mioyo Na Nyumba Za Ibada Na Wahudumu Wote)-Ninaalika Moto Wa Roho Mtakatifu Uende Katika Misikiti, Makanisa, Maduka Na Maeneo Yote Ya Biashara; Ikiwemo Katika Mahoteli, Sokoni, Mashambani, Na Madukani; Katika Barabara Kuu Na Katika Njia Panda Zote! Kwa Jina La Yesu Kristo Mwana Wa Mungu Aliye Hai, Kazi Zote Za Shetani, Wajumbe Wa Kuzimu Mapepo Na Roho Zote Zihamishwe, Ziharibiwe, Na Ninazitupia Kuzimu Zifungwe Zisiletwe Tena Duniani! Ninazialika Nguvu Za Mungu Na Ushuhuda Wa Roho Mtakatifu Pamja Na Miujiza Ya Mungu Aliye Hai Milele Na Milele Ikatawale Katika Jina La Yesu Kristo Mwana Wa Mungu Aliye Hai Mile Na Milele Amina!
7. Sasa - Ninakusifu, Ninakuabudu, Na Kukuinua Mungu Wangu Uliye Hai, Katika
Jina La Yesu.
Ni Kwa Neema Yako Mungu Katika Roho Mtakatifu Na Kupitia Bwana Yesu Kristo; Sasa Niko Tayari, Kukusifu, Kukuinua, Kukuabudu. Kwa Maana Wewe Umenijaza Nguvu Na Umenipaka Mafuta Mapya Ya Nguvu Mpya, Ili Kuzishinda Nguvu Zote Za Shetani Na Majeshi Yake Ya Pepo Wabaya; Pamoja Na Dhambi Na Udhaifu Wote! Umenifanya Sasa Na Utaendelea Kunifanya Kuwa Chombo Kilicho Tayari Kwa Ajili Ya Utukufu Wako Milele, Ee, Mungu; Hebu Sasa Ninaomba Uniwezeshe Tena, Nikusifu, Nikuinue Na Kukuabudu Mungu Katika Uzuri Wa Utakatifu Wako! Na Tazama Umesema Katika Zaburi Ya 29:1.2; ya kuwa Tukupe Utukufu Wa Jina Lako, Na Tene Tukuabudu Kwa Uzuri Wa Utakatifu Wako; Asante Sana Mungu Wetu, Katika Utakatifu Wa Utatu Wako!
Ni Kwa Neema Yako Mungu Katika Roho Mtakatifu Na Kupitia Bwana Yesu Kristo; Sasa Niko Tayari, Kukusifu, Kukuinua, Kukuabudu. Kwa Maana Wewe Umenijaza Nguvu Na Umenipaka Mafuta Mapya Ya Nguvu Mpya, Ili Kuzishinda Nguvu Zote Za Shetani Na Majeshi Yake Ya Pepo Wabaya; Pamoja Na Dhambi Na Udhaifu Wote! Umenifanya Sasa Na Utaendelea Kunifanya Kuwa Chombo Kilicho Tayari Kwa Ajili Ya Utukufu Wako Milele, Ee, Mungu; Hebu Sasa Ninaomba Uniwezeshe Tena, Nikusifu, Nikuinue Na Kukuabudu Mungu Katika Uzuri Wa Utakatifu Wako! Na Tazama Umesema Katika Zaburi Ya 29:1.2; ya kuwa Tukupe Utukufu Wa Jina Lako, Na Tene Tukuabudu Kwa Uzuri Wa Utakatifu Wako; Asante Sana Mungu Wetu, Katika Utakatifu Wa Utatu Wako!
a) Sura Na Umbile Lako Mungu; Wewe Mungu Ni Roho Tena Mtakatifu Wa Watakatifu; Ni Wa Milele Uliyekuwako, Uliyeko, Na Utakayekuja. Wewe Ni Mkuu Sana, Huna Mipaka Wala Kizuizi. Uzima Wako Ni Wa Milele Na Milele Yote.
b) Uweza Wako Mungu Ni Wa Ajabu Ya Kutisha; Una Uweza Wa Milele Na Milele. Unaweza Yote, Wala Hauchoki! Unajua Yote, Hekima Na Maarifa Yako Havichunguziki, Uko Popote, Mahali Pote Kwa Wakati Wote – Hulali Wala Husinzii! Uwepo Wako Huleta Utukufu, Umeijaza Mbingu Na Nchi, Tena Unapendeza Na Kutisha Kama Nini! Unamiliki Vyote, Dunia Na Vyote Viijazavyo, Pamoja Na Mbingu Na Majeshi Yako Yote, Vyote Ni Vyako!
c) Tabia Zako Mungu Na Mwenendo Wako Pia Havichunguziki! Na Wala Hakuna Lugha Itoshayo Kuelezea Uzuri Wako! Maana Msimamo Wako Ni Wa Milele Katika Utakatifu Wa Utakatifu Wote! Wewe Mungu Unatenda Mema, Kwako Hakuna Tendo Lolote Baya Kamwe! Huna Kigeugeu Wala Kivuli Cha Kugeuka Geuka – Haubadiliki Kamwe Msimamo Wako! Umejaa Huruma, Rehema, Na Fadhili Za Milele Na Upendo Wa Milele! Ni Mungu Mwenye Utukufu Mwingi.
d) Mapenzi Yako Ni Mema! Wewe Mungu Unapenda Mema Na Unachukia Dhambi Na Ubaya Wote! Ni Mungu Unayetuwazia Mema Siku Zote, Maneno Yako Na Matendo Yako Kwetu Ni Kwa Mapenzi Yako Mema – Nasi Katika Hayo Yote Tunauona Uzuri Wako Mkuu Ajabu! Unayakubali Mema Na Kuyakataa Mabaya Yote! Unachukia Mabaya Na Dhambi Za Waovu, Bali Unawapenda Viumbe Wako Wote, Wema Na Wabaya! Kwa Neno Lako Umetujulisha Mapenzi Yako Kwamba-Hakuna Atakayetutenga Na Upendo Wako Mungu!
e) Jina Lako Ni Kuu, Takatifu Sana, Na Tukufu Sana.Linauweza Na Nguvu Za Milele. Lina Mamlaka Yote. Ni Ngome Na Thawabu Kubwa Sana Kwa Kila Akuaminiye – Kwa Uponyaji, Ulinzi, Msaada, Na Wokovu; Tena Ni Silaha Bora Sana! Wewe Ni Yehova Elshadai, Wewe Ni Yehova Nisi, Yehova Rafa, Yehova Shama, Yehoha Yire.... !
f) Njia Zako ( Kawaida, Desturi, Kanuni, Taratibu, Siri, Amri, Na Mapito Yako Yote) Hazichunguziki, Hazitafutikani, Hazifananishwi! Ni Za Hekima Na Maarifa Makuu Sana Kupita Wote! Wewe Ni Mungu Wa Maagano Na Kweli.
g) Neno Lako Ni La Milele, Halina Makosa, Hata Hivyo Tazama; Umelihakikisha Tena Mara Saba! Ni Uzima, Ni Nuru, Ni Taa Na Mwangaza Kwetu, Ni Kali Kuliko Upanga Uwao Wote Ukatao Kuwili.
h) Kazi Zako Na Huduma Zako Kwa Wote Zaonakana Na Zatambulikana Kuwa Ni Za Heshima Na Adhama Kuu. Na Tena Ni Kuu Na Za Ishara Maajabu Na Miujiza Mikuu. Unaokoa Na Kukomboa – Wewe Ni Shujaa Wa Wema Wote! Uumbaji Wako Ni Mkuu Wapendeza Sana. Unatoa Karama Na Huduma Zako Kwa Wanadamu Tuwe Mawakili Tu! Unazivunja Na Kuziharibu Kazi Zote Za Shetani Ili Kututetea Na Kutuponya Wanadamu Tusionewe Na Kuharibiwa Na Shetani – Tena Na Tazama, Umetupa Amri Na Uwezo Wa Kukanyaga Nyoka Na Nge Na Nguvu Zote Za Yule Mwovu, Wala Hakuna Kitakacho Tudhuru! Kazi Zako Zinapendeza, Unazozitenda Ndani Ya Watu Kupitia Watu Wote Na Hasa Wale Walioitwa Kwa Jina Lako! Wewe Ni Mungu Uletaye Neema, Kweli Na Uzima Wa Milele Kupitia Mwanao Na Bwana Wetu Yesu Kristo.
i) Unastahili Wewe Bwana. Kujulikana Mbinguni Na Duniani Kote Kuwa Ndiwe Mungu Pekee! Utukufu Wote, Heshima Zote, Adhama, Ukuu, Enzi Na Mamlaka Yote! Kusifiwa, Kuinuliwa, Kuabudiwa Na Kutukuzwa Milele Kuliko Wote Na Kupita Miungu Yote. Kumiliki, Kutamalaki, Kutawala Vyote Milele!
NAAMINI UMEPATA KITU KUTOKA KATIKA MAOMBI HAYA MUNGU AKUBARIKIII SANA
JE WATAKA KUVUKA NA KUTAWALA
Watu wengi tunajua ya kuwa MUNGU alituumba ili tumilki na kutawala. Kitu kilicho sababisha hata sasa hatufanikwi ni kule kutotii sauti ya MUNGU na jambo hili limefanya
watu kutosonga mbele kimaisha maana neno la MUNGU linasema katika Joshua 1:8
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari
maneno yake mchana na usiku upate kuangalia na kutenda sawaswa na maneno
yote yaliyoandikwa humo, maana ndipo utakapofanikisha njia yako kisha ndipo utakapostawi sana.
Je ndani yako ndani yako kunalo neno la Mungu? Wakristo wengi wamejisahau hata kusoma neno la MUNGU,
unakuta mkristo muda mwingi yuko WhatsAp, Facebook, wasengenyaji n.k.
Na watu hawa ndio mara nyingi utawaona wako rohoni kumbe hao ndio
waharibifu wa
kazi ya MUNGU. Watu wengi wanajikuta wamewaamini hawa watu
na kuwapa mambo yao ya siri halafu wanayakuta yamezagaa mitaani wasijue kua Siri zao wamepeleka sehemu isiyo sahihi. Sababu kuwa mwana wa MUNGU nikuwa mbeba siri za MUNGU kwa hiyo watu hawa wamekuwa
kidonda katika kazi ya Mungu na hii imekua ikurudisha nyuma kazi ya MUNGU.
Na watu hawa wamekuwa wakipatwa na magonjwa yanayo sababishwa na uchungu wa ndani (yaani lile jambo ulilolibeba moyoni ). Biblia inasema MITHALI
14:30a Moyo ulio mzima
ni uhai wa mwili . Je hawa wapendwa feki wanaua watu wangapi kwenye
makanisa wanayosali? Kama na wewe upo katika kundi
hilo tambua biblia inasema katika Luka17:2 Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmoja wa wadogo hawa. Je kunayo sababu ya wewe kusema kuwa nimeokoka! badilika tambua kuwa unavyofanya MUNGU hapendezwi na wewe na shetani anakushangaa.
Tambua kuwa bado unayo nafasi ya kutengeneza na Bwana MUNGU
wako, nenda mbele za MUNGU mwabie baba nimekosa tamka makosa yako bila kuficha mbele za MUNGU sababu Mithali 11:7
inasema Mtu mwovu atakapokufa, taraja lake
lapotea; na matumaini ya uovu huangamia. Kwahiyo inapasa kuungama
dhambi zote.Wala Usiache hata moja kwa kuhofia watu wanasikia endelea kumsihi
MUNGU wako naye atakusamehe.
Ukisoma ZABURI 51:7 Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi,
Unioshe, nami nitakuwa mweupe kama theluji, hii ina maana kwamba dhambi zako zitakuwa mbali na wewe na
wakati huo utaanza kuisikia sauti ya MUNGU ikikuongoza katika Jina lipitalo majina yote, jina la YESU.
MUNGU AWABARIKI KWA KUWEZA KUTUMIA MUDA WAKO KUJIPATIA UFAHAMU KATIKA NENO LA
MUNGU
MCH FRANK MINJA
CONT +255758338594
Very powerful am totally blessed
ReplyDeletenimebarikiwa sana sana.
ReplyDeleteAmen
DeleteNimebarikiwa sasa nashukuru Sana
ReplyDeleteAm really blessed
ReplyDeleteAm encourage and empowered thank you
ReplyDeleteKeep up many will see deliverance
ReplyDeleteGreat 👍 and wonderful.
ReplyDelete