Thursday, July 30, 2020
Filled Under:
Socialize It →
|
|
MAPAMBANO YA VITA VYA NDOTO
Mathayo 16
19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
Isaya 54
17 Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.
Mathayo 15
13 Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litangolewa.
Baba ninalileta lango la ndoto na maono mbele zako, ninatubu na kuomba Rehema kwa ajili ya hili lango katika jina la Yesu, ninatubu na kuomba Rehema kwa ajili ya roho yangu, nafsi yangu na mwili, mahali popote ambako sikuyafanya mapenzi yako ninatubu nakuomba Rehema, nanyunyiza damu ya Yesu juu ya nafsi yangu, mwili wangu na roho yangu, najitakasa kwa damu ya Yesu, Baba kila mashitaka na hukumu kinyume na maombi haya ninasimama ba damu ya Yesu, ninafuta hayo mashitaka na hukumu zake kwa damu ya Yesu katika jina la Yesu. Ee Mungu uliyehai imeandikwa tumbo langu litakula matunda ya kinywa changu, pia imeandikwa baraka na laana vipo katika uweza wa ulimi. imeandikwa lolote nitakalolifunga hapa duniani litafungwa litafungwa hata huko mbinguni na lolote nitakalo lifungua hapa duniani litafunguliwa hata mbinguni, Baba katika jina la Yesu, Mchawi anayewaamsha wenzake kwa filimbi ili wakaloge katika mtaa wangu ninamfunga kwa damu ya Yesu, ninampiga na radi ya Roho Mtakatifu miali ya moto ikamuunguze na kumuangusha chini katika jina la Yesu, ninaamuru filimbi anayopiga igeuke kuwa moto ikamuunguze mdomo wake, na sauti yake ikampasue masikio yake mwenyewe asisikie ububu na ukiziwi ukampate katika jina la Yesu,kuanzia leo hii yoyote anayekuja katika umbo la fumbo katika ndoto, yeye anayekuja kama mnyama, kama mdudu, kama ndege,ama kwa sura ya mtu mwingine ninamfunga kwa damu ya Yesu, ninavua sura yake ya kutengeneza kwa damu ya Yesu, ninamvika sura yake ya asili sasa kwa damu ya Yesu, ninaamuru macho yangu yafunguke nimwone katika sura yake na umbo lake la asili katika jina la Yesu, kwa damu ya Yesu naharibu roho ya makengeza nalifunga pepo la makengeza katika ndoto katika jina la Yesu,kwa damu ya Yesu, nguvu ya makengeza naipasua kwa damu ya Yesu, Baba anayekuja katika umbo la kutengeneza kuanzia leo hii nitamwona katika umbo lake la asili katika jina la Yesu, ninaharibu kwa damu ya Yesu maumbo feki ninayabomoa maumbo yao katika jina la Yesu, Baba sura yangu ninaifunuka kwa damu ya Yesu, ninaitakasa kwa damu ya Yesu, kuanzia leo hii sura yangu mimi haitatumika na wachawi atakayejaribu kuvua sura yangu kichawi na kuivaa kichawi naamuru moto wa Roho Mtakatifu ukaungushe sura yake yote aungue uso mzima katika jina la Yesu, Baba ninawafunga wachawi wote walogao kwa kikundi kwa damu ya Yesu, ninawapiga upofu watakapokuja wasinione katika jina la Yesu, kila anayekuja kuniloga ninaamuru akwame asirudi katika mwili wake katika jina la Yesu, ninampiga upofu asione njia aliyoijia katika jina la Yesu,sura yangu mimi ninaunganisha na sura ya Yesu, katika jina la Yesu, mchawi yoyote atakayenitazama moto wa Roho Mtakatifu umuunguze na kumpofua macho yake katika jina la Yesu, Baba kuanzia leo hii kila matukio ya kichawi, maumbo ya kichawi, ramani za kichawi zilizotengenezwa kinyume na mimi ,ili ninapoamka toka ndotoni nisahau ndoto, ndoto ipeperuke, maono yayeyuke, nisiamke kuomba bali nilale tena, au nishindwe kuomba baada ya kuota ndoto, au nipuuzie ndoto, ninafuta kwa damu ya Yesu, anayehusika kusimamia hayo leo ninashindana na wewe kwa damu ya Yesu, nafanya vita kwa damu ya Yesu, nakufunga kwa jina la Yesu, wewe unayeiba ndoto zangu, wewe unayefanya nisahau ndoto, wewe unayefanya nisiombee ndoto wewe mkuu wa anga eneo nalokaa, wewe mkuu wa nchi,wewe mkuu wa bahari ninakufunga kwa damu ya Yesu, ninakuharibu kwa jina la Yesu, ninaachilia upanga ukufyeke kwa jina la Yesu, wewe unayeniletea ndoto mbaya zenye mafumbo ili kuniingiza katika maagano, kunifunga kwenye viapo, huna mamlaka mamlaka anayo Yesu ninakufunga leo hii kwa jina la Yesu, wewe unayenichimbia shimo, wewe unayenitegea mitego, wewe unayepanda pando la kichawi juu yangu, wewe unayebomoa boma la Bwana, wewe mchawi, wewe mshirikina, wewe mganga wa kienyeji, wewe unayejigeuza buibui, unayejigeuza mjusi, unayejigeuza nzi, unayejigeuza mbu, unayejigeuza mbwa, unayejigeuza paka, unayejigeuza ndege, wewe uliyeingia ndani yangu kupitia mlango wa ndoto na kujigeuza laana, mikosi, balaa, kujigeuza vimbe za tumbo, imeandikwa Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji,Na katika tauni iharibuyo.Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao. Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana, Wala tauni ipitayo gizani,Wala uele uharibuo adhuhuri, Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume!Hata hivyo hautakukaribia wewe. Ila kwa macho yako utatazama,Na kuyaona malipo ya wasio haki. Neno la Mungu ni upanga wa roho imeandikwa utaanguka mkono wangu wa kuume, leo ninawafyeka kwa damu ya Yesu, ninaachilia upanga wa neno la Mungu, ninakufyeka kwa jina la Yesu, nakufyeka ewe mchawi mwanaume, ewe mchawi mwanamke katika jina la Yesu. kila uliyoyapanda kwangu kupitia mlango wa ndoto na maono imeandikwa kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litangolewa, leo hii ninaachilia damu ya Yesu juu ya mapando yote ya kichawi, pando kupitia kula ndotoni, pando la aibu, pando la fedheha, pando la umasikini, pando la magonjwa, pando la hasara, pando la ajali, pando katika hatua zangu, pando katika vibali vyangu, pando lolote ninalolijua nisilolijua ninalingoa kwa damu ya Yesu, popote lilipo pando la waziwazi au sirini ninayangoa kwa damu ya Yesu, katika jina la Yesu, Baba kila silaha iliyofanyika kinyume changu kupitia ndoto natamka kutokufanikiwa, natamka kuanguka, natamka kushindwa katika jina la Yesu, nanyamazisha silaha zao kwa damu ya Yesu, nazifunga Silaha zao kwa damu ya Yesu katika jina la Yesu, kuanzia leo hii adui atakapo kuja kwa njia ya ndoto nitamwona katika umbo lake la asili katika jina la Yesu, kuanzia leo hii nikiamka sitasahu ndoto niliyoiota kwa jina la Yesu, kuanzia leo hii ndoto zangu hazitapeperuka kwa jina la Yesu, nazizungushia ndoto zangu kwa ukuta wa damu ya Yesu, kuanzia leo hii nitakapo amka kushituka katika ndoto nitaomba hapohapo sitalala tena katika jina la Yesu, kuanzia leo nitakumbuka ndoto nazoota kwa jina la Yesu, nanyunyiza damu ya Yesu kwenye kumbukumbu zangu za rohoni na mwilini katika jina la Yesu, kuanzia leo hii wachawi wote wanaokuja njia ya ndoto nitawaona nitawafunga na kuwapiga na kuwashinda ndotoni katika jina la Yesu. ndoto za kipepo zinazokuja baada tuu ya kuota ndoto ya Mungu, kuanzia leo hii nazifunga kwa damu ya Yesu, madhara yoyote yaliyowahi nipata sababu ya ndoto mbaya kuanzia leo nimeyafuta kwa damu ya Yesu,madhara yatawapata hao adui zangu na hao wanichukiao katika jina la Yesu, kila laana waliyonitamkia ndotoni Baba haitafanya kazi kwangu katika jina la Yesu, Baba naomba ukageuze laana zao kuwa baraka kubwa kwangu ili wanaonifanyia mabaya kwa kificho wapatwe na fedheha na aibu katika jina la Yesu, Baba ninafyatua mitego yao kwa damu ya YESU, ninafuta manuizo yao yote waliyoninuzia kwa jina la Yesu, ninaharibu mipango yao yote kwa damu ya Yesu, Baba kama vile ulivyomrejesha mnyweshaji wa Farao katika nafasi yake naomba Baba uachilie ndoto itakayonirejesha kwenye hatima yangu katika jina la Yesu, Baba kama vile ulivyombariki Suleimani na kubadili maisha yake naomba uachilie ndoto itakabadilisha maisha kama Suleimani katika jina la Yesu, Baba kama vile ulivyompelekea labani, ulivyompelekea Abimaleki utisho Ee Bwana ukawapekee ndoto za kitisho adui zangu na watesi wangu ndoto za utiisho katika jina la Yesu, Baba kama ulivyomletea Gidioni ndoto ya habari njema naomba Bwana uniletee ndoto ya habari njema ya kunipa tumaini katika jina la Yesu. Baba nakushukuru kwa kuwa umesikia na umefanya zaidi ya nilivyoomba na kufikiri katika jina la Yesu Amen.
Mch Frank Minja
Cont+255673776380
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Translate
Kilimanjaro House Of Prayer 2007. Powered by Blogger.
About Me
Search This Blog
Categories
Labels
Popular Posts
-
JINSI YA KUOMBA ( MAOMBI YA HATARI. EFESO 6:10 Hatimaye ndugumzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uwez...
-
Watu wengi tunajua ya kuwa MUNGU alituumba ili tumilki na kutawala. Kitu kilicho sababisha hata sasa hatufanikwi ni kule kutotii sauti ya M...
-
MAPAMBANO YA VITA VYA NDOTO Mathayo 16 19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa li...
0 comments:
Post a Comment