Saturday, April 27, 2019

Prayer Of The Righteous Man

Wednesday, April 24, 2019

JE WATAKA KUVUKA NA KUTAWALA

Watu wengi tunajua ya kuwa MUNGU alituumba ili tumilki na kutawala. Kitu kilicho sababisha hata sasa hatufanikwi ni kule kutotii sauti ya MUNGU na jambo hili limefanya watu kutosonga mbele kimaisha maana neno la MUNGU linasema katika Joshua 1:8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku upate kuangalia na kutenda sawaswa na maneno yote yaliyoandikwa humo, maana ndipo utakapofanikisha njia yako kisha ndipo utakapostawi sana. Je ndani yako ndani yako kunalo neno la Mungu? Wakristo wengi wamejisahau hata kusoma neno la MUNGU, unakuta mkristo muda mwingi yuko WhatsAp, Facebook, wasengenyaji n.k. Na watu hawa ndio mara nyingi utawaona wako rohoni kumbe hao ndio waharibifu wa kazi ya MUNGU. Watu wengi wanajikuta wamewaamini hawa watu na kuwapa mambo yao ya siri halafu wanayakuta yamezagaa mitaani wasijue kua Siri zao wamepeleka sehemu isiyo sahihi. Sababu kuwa mwana wa MUNGU nikuwa mbeba siri za MUNGU kwa hiyo watu hawa wamekuwa kidonda katika kazi ya Mungu na hii imekua ikurudisha nyuma kazi ya MUNGU. Na watu hawa wamekuwa wakipatwa na magonjwa yanayo sababishwa na uchungu wa ndani (yaani lile jambo ulilolibeba moyoni ). Biblia inasema MITHALI 14:30a Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili . Je hawa wapendwa feki wanaua watu wangapi kwenye makanisa wanayosali? Kama na wewe upo katika kundi hilo tambua biblia inasema katika Luka17:2 Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmoja wa wadogo hawa. Je kunayo sababu ya wewe kusema kuwa nimeokoka! badilika tambua kuwa unavyofanya MUNGU hapendezwi na wewe na shetani anakushangaa. Tambua kuwa bado unayo nafasi ya kutengeneza na Bwana MUNGU wako, nenda mbele za MUNGU mwabie baba nimekosa tamka makosa yako bila kuficha mbele za MUNGU sababu Mithali 11:7 inasema Mtu mwovu atakapokufa, taraja lake lapotea; na matumaini ya uovu huangamia. Kwahiyo inapasa kuungama dhambi zote.Wala Usiache hata moja kwa kuhofia watu wanasikia endelea kumsihi MUNGU wako naye atakusamehe. Ukisoma ZABURI 51:7 Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kama theluji, hii ina maana kwamba dhambi zako zitakuwa mbali na wewe na wakati huo utaanza kuisikia sauti ya MUNGU ikikuongoza katika Jina lipitalo majina yote, jina la YESU. MUNGU AWABARIKI KWA KUWEZA KUTUMIA MUDA WAKO KUJIPATIA UFAHAMU KATIKA NENO LA MUNGU MTUMISHI FRANK MINJA.